Monday, July 18, 2011

Kongamano Mzumbe lafana May 20, 2011

Wakuu, Habari za Ijumaa.

Ni mataumaini yangu kuwa mnaendelea salama na shughuli zenu za kila siku.

Napenda kutumia jukwaa hili kuwataarifu kuwa kesho tarehe 21 Mei 2011 kutakuwa na Kongamano la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Katika Kongamano hilo Dr Slaa ndiye mgeni rasmi ambapo atazungmza na wanazuoni hao kwa pamoja wakijadili mustakabali wa Taifa la Tanzania. Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 4 asubuhi katika Ukumbi wa Paradise Mzumbe. Mada mbalimbali zitajadiliwa.

Pamoja na Dr Slaa, Makamanda wengine wa CHADEMA watakaokuwepo ambao ni Fredy Mpendazoe, John Mrema, Benson Kigaila na Regia Mtema ninayecheza uwanja wa nyumbani.

Pamoja na kuhudhuria Kongamano la kesho lakini pia leo baadhi yetu tutahudhuria Kongamano la Katiba lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe litakalofanyika Chuoni hapo kuanzaia saa 3 asubuhi.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Morogoro Mjini
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

================================
KATIKA PICHA:




No comments:

Post a Comment