Ndugu zangu habari!!
Kwanza kabisa niwapongeze kwa shughuli zenu na mijadala mbalimbali humu jamvini.
Natambua kwamba nilikuwa nanyi nikiwa mwanachama hai wa JF kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Kipindi hicho nilikuwa natumia jina la siri ambalo watu wachahche sana walinitambua. Mwezi Julai mwaka huu baada ya kushinda kura za maoni ilinibidi nitumie jina langu halisi nikiwa kama mgombea Ubunge Jimbo la Kilombero-Morogoro.
Sasa nipo kwenye maisha mapya zaidi, maisha ya Ubunge. Kwa muda mfupi nilioanza kuishi maisha ya Ubunge kuna mambo nimeanza kujifunza, kifupi mengine yananiboa.
1. Nahitajika kuwa na Makazi ya kudumu matatu: Dodoma, Kilombero na Dar - Inanikera
2. Kila mmoja anataka nisave namba ya simu yake kwenye simu yangu-sijui ninunue simu ya ukubwa gani ili wote waingie.
3. Natakiwa kubadilisha vijiwe, nikibadilisha wengine hawatanielewa.
4. Appointments zimeanza kuwa nyingi
5. Usipopokea simu kwa sababbu zinazoeleweka unatafsiriwa vibaya kwa mfano uko kwenye kikao au mbali na simu.
Hizi ni baadhi ya changamoto nilizoanza kukumbana nazo.
Nawasilisha........
No comments:
Post a Comment