Monday, July 18, 2011

Chadema Yatikisa Mbeya, Machi 6, 2011

Wakuu,

Hivi sasa ndio tunajipanga ili kuanza Maandamano yetu. Mji umejaa hamasa kubwa kila ukipita bendera za CHADEMA na ishara ya vidole viwili ndio vimetawala.

Watu wamependeza sana na Kombati na Sare nyingine za Chama. Tunatarajia kuanza Maandamano mida ya saa sita. Magari yote ya msafara yako hapa Forest yakipiga nyimbo mbalimbali za chama. Maandamano yanatarajiwa kuanza maeneo ya Mafiat njia ya Uwanja wa Ndege yataelekea Viwanja vya Ruandanzovwe Mwanjelwa.

Leo tutatembea Kilomita Mbili tu.

Pata picha za Awali.







Aluta Continua
Kutoka Mbeya Forest

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

No comments:

Post a Comment