Monday, July 18, 2011

Chadema watembelea Kaburi la Baba wa Taifa - Butiama Feb 27, 2011

Wakuu,

Baada ya kuingia Musoma na kufanikiwa kufanya maandamano kwa amani na utulivu mkubwa leo vikosi vitatembelea Wilaya za Mkoa huu. Lakini kabla ya kwenda kwenye wilaya, Viongozi wote tukiongozwa na Kamanda Mbowe tutaelekea kuzuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuweka mashada ya maua.

Vikosi leo vitaelekea Tarime, Rorya, Bunda, Serengeti, Mwibara na Musoma Vijijini.

Hauna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Musoma

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

No comments:

Post a Comment