Wakuu, Habari!!!
Yale Maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa yanatarajiwa kuhitimishwa leo kwa maandamano makubwa na ya aina yake Bukoba Mjini. Maandamano hayo yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.Maandalizi yameshakamilika na msafara wa Vikosi Kazi ndio unajiandaa kutoka Kahama vilipotia nanga kuelekea Bukoba. Kazi kamili itahitimishwa kesho kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye Wilaya za Mkoa wa Kagera. Baada ya hapo Vikosi vitarudi Dar es salam kwa maandalizi ya Kanda nyingine baada ya Bunge la Aprili. Habari ya matukio baadaye kazi ikianza.
Kutoka Kahama
Regia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.
=================
KATIKA PICHA
Hapa ni Kemondo
Hapa ni Rwamishenye![]()
Last edited by Regia Mtema; 2nd March 2011 at 06:19 PM.
No comments:
Post a Comment